Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alkaadhim (a.s) katika ukanda wa kijani

Mradi wa ukanda wa kijani kusini mwa Karbala chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, umefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alkaadhim (a.s).

Kiongozi wa Majmaa bwana Naasir Hussein Mut’ibu amesema “lengo la majlisi hii ni kutoa mawaidha na maelekezo kwa watumishi sambamba na kuelimisha wakazi wengi wa maeneo haya”.

Akaongeza kuwa “Kufanya majlisi za kuomboleza katika vitongoji hivi ni mwanzo wa utekelezaji wa ratiba ya kitamaduni kwa watumishi na wakazi wote kwa ujumla”.

Mhadhiri wa majlisi shekhe Abdul-Amiir Almansuri amesema “Lengo la kufanya majlisi katika miji hii iliyobadilishwa kutoka jangwa na kuwa kijani kibichi, ni kuhuisha alama za Mwenyezi Mungu na kufanyia kazi kauli isemayo (wanafurahi kwa furaha zetu na wanahuzunishwa kwa huzuni zetu)”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Almansuuri “Majlisi za kuomboleza zinamaanisha kuwa popote tulipo hatuwezi kusahau mambo ya kitamaduni na utukufu wa Ahlulbait (a.s), kila tunacho fanya ni katika baraka za Maimamu watakasifu (a.s), na tunachofanya ni kidogo ukilinganisha na utukufu wao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: