Chuo kikuu cha Al-Ameed kimeadhimisha historia ya Imamu Mussa bun Jafar Alkaadhim (a.s) na msimamo wake wa milele mbele ya matwaghuti wa zama zake, kufuatia maombolezo ya kifo chake (a.s).
Chuo kimefanya majlisi ndani ya ukumbi wa Imamu Almujtaba (a.s) kwa ushiriki wa watumishi na wanafunzi wa chuo.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo somwa na mwanafunzi kutoka kitivo cha udaktari Mussa Ahmadi, kisha akapanda kwenye mimbari Mheshimiwa Shekhe Ali Saidi, akaongea kuhusu historia takatifu na jihadi kubwa ya Imamu Mussa bun Jafari Alkaadhim (a.s), na mateso aliyopata katika jela za Haruna Rashidi, pamoja na kueleza uvumilivu wake hadi alipo uawa kwa sumu (a.s).
Majlisi ikahitimishwa kwa kusomwa tenzi za huzuni na Ali Aljaabiri zilizo eleza dhulma alizofanyiwa Imamu (a.s) ndini ya magereza.