Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya hafla kubwa ya kuadhimisha kumbukumbu ya kupewa Utume kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) katika mji wa Sanjaar kwenye mkoa wa Nainawa.
Hafla hiyo imeandaliwa na kituo cha utamaduni na maendeleo endelevu katika idara ya maelekezo ya kidini chini ya kitengo.
Kiongozi wa idara Shekhe Haidari Aaridhi amesema “Tumefanya hafla kubwa kufuatia kumbukumbu ya kupewa Utume kwa Mtume wetu mtukufu katika wilaya ya Sanjaar, chini ya maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuhuisha matukio ya kidini”.
Akaongeza kuwa “Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyosomwa na Saalim Muhammad Saidi, ikafuatiwa na mawaidha yaliyo fafanua umuhimu wa kuhuisha matukio ya kihistoria katika Dini ya kiislamu, kisha ukafuata ujumbe wa rais wa muungano wa mashia wa Sanjaar Sayyid Mahmuud A’raji”.
Hafla ilikuwa na vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na uimbaji wa qaswida kutoka kwa mwimbaji mashuhuri Ahmadi Salam Karbalai, mashindano ya kidini, na kutoa zawadi kwa washindi.