Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kazi ya kusafisha mto wa Husseiniyya na kuuweka katika mazingira mazuri.
Makamo rais wa kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) Mhandisi Mahadi Muhammad Mussawi amesema “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu yanayo himiza kusaidia juhudi za serikali, wahudumu wa kitengo chetu wanashirikiana na idara ya maji kusafisha mto wa Husseiniyya”.
Kazi ya kusafisha mto imeanzia katika eneo la jirani na Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f), tunaondoa taka zinazokwamisha utembeaji wa maji na kuyafanya maji yatembee vizuri bila kizuwizi chochote sambamba na kuuweka mto katika muonekano mzuri.