Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amesema: Zaidi ya tani 1555 za chakula zitatumwa kwa waathirika wa tetemeko nchini Sirya.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Murtadha Aali Dhiyaau-Dini amesema kuwa zaidi ya tani (1555) za chakula zitatumwa kwa waathirika wa tetemeko nchini Sirya, katika msafara wa kwanza wa Ataba tukufu.

Mheshimiwa katibu mkuu amesema “Kutokana na utekelezaji wa maagizo ya Marjaa Dini mkuu na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, tumekamilisha maandalizi ya kutuma msafara wa kwanza wa shehena ya chakula zaidi ya tani (1555) kwa waathirika wa tetemeko nchini Sirya”.

Akaongeza kuwa “Msafara huo utakuwa na watu zaidi ya 220 watakao toa huduma za kibinaadamu kama chakula, dawa, ufungaji wa mahema kwa watu waliopoteza nyumba zao kutokana na tetemeko sambamba na ugawaji wa tani 108 wa vifaa vya umeme, aidha kuna uwezekano wa kutuma msafara mwingine wa misaada baada ya kukamilika hatua hii”.

Akabainisha kuwa “Shehena hiyo ya misaada itasafirishwa kupitia maroli 76 yenye ukubwa tofauti, yatakayo saidia kufikisha msaada kwa haraka kadri itakavyo wezekana”.

Kwa mujibu wa maelezo ya kazibu mkuu: “Msaada wa Atabatu Abbasiyya kwa ndugu zetu raia wa Sirya, unafuatia tetemeko lililo sababisha maafa makubwa kusini mwa nchi ya Sirya”, akabainisha kuwa “Atabatu Abbasiyya huwa mstari wa mbele kusaidia waathirika wa majanga mbalimbali kwenye maeneo tofauti ndani au nje ya Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: