Balozi wa Hispania nchini Iraq apongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya na huduma zake kwa mazuwaru

Balozi wa Hispania nchini Iraq Mheshimiwa Bedru Martinzi amepongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya na huduma wanazopewa mazuwaru.

Mheshimiwa Martinzi alipokutana na katibu mkuu Sayyid Mustafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amesema “Nimefurahi sana kuona idadi kubwa ya watu wanaokuja kufanya ziara sehemu hii tukufu, inayokusanya watu wa Dini tofauti na madhehebu tofauti, nimefurahishwa sana na mazingira ya kiroho yaliyopo katika mji wa Karbala”.

Akaongeza kuwa “Nilisoma kisa cha Imamu Hussein na ndugu yake Abbasi (a.s) namna walivyo jitolea kwa ajili ya kunusuru misingi ya ubinaadamu, kujitolea mhanga ndio sababu ya watu kutoka kila sehemu ya dunia huja hapa kufanya ziara”

Balozi akapongeza mapokezi mazuri aliyopewa na wahudumu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, aidha amevuliwa na mali zinazomilikiwa na Ataba tukufu sambamba na huduma zinazotolewa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: