Jumuiya ya Al-Ameed imetoa wito wa kushiriki kwenye kongamano la kielimu la fikra ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s).
Kongamano litafanywa chini ya anuani isemayo (Imamu Hassan “a.s” mrithi wa nyumba ya Utume), chini ya ufadhili wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kwa usimamizi wa kamati kuu ya mradi wa Hilla mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), chuo kikuu cha Baabil, Jumuiya ya Al-Ameed na chuo cha Alkafeel na Al-Ameed.
Jumuiya ilianza kupokea mada zitakazo wasilishwa kwenye kongamano hilo toka tarehe 15/2/2023m, tarehe ya mwisho ya kupokea mada hizo ni (15/5/2023m).
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa barua pepe au tupigie simu namba: 009647602323337