Watumishi wa idara ya usimamizi wa haram ya Atabatu Abbasiyya wameweka mauwa kwenye haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kuingia kwa mwezi wa Shabani.
Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Nizaar Ghani Khaliil amesema: “Kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Shabani, wahudumu wetu kwa kushirikiana na idara ya Masayyid wameweka mapambo yanayo onyesha muonekano wa furaha kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika miezi hii mitukufu”.
Akaongeza kuwa “Mauwa yaliyotumika yameagizwa kutoka nje ya nchi kutokana na kutopatikana kwa aina hiyo hapa nchini” akabainisha kuwa “Yamewekwa kwa namna ambayo yataendelea kubaki na muonekano mzuri kwa muda mrefu”.
Akaendelea kusema “Marashi na mauwa mazuri yatagawiwa kwa mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Maimamu watakasifu (a.s)”.