Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza kuanza kwa shindano la kitamaduni awamu ya pili, linalohusu mazazi ya watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani hususan Abulfadhil Abbasi (a.s).
Majina ya washindi kumi wa mwanzo yatatangazwa siku ya Alkhamisi (23/2/2023) saa moja jioni kwenye mitandao ya kijamii iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Sharti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla itakayofanywa katika eneo la mlango wa Kibla ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Ijumaa (24/2/2023) saa moja jioni.
Kesho litatolewa tangazo maalum awamu ya tatu la kuzaliwa kwa Imamu Zainul-Aabidina (a.s).