Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza majina ya washindi wa shindano la (watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani) hususan mazazi ya Imamu Hussein (a.s).
Uongozi mkuu wa Ataba tukufu umesema, Zawadi zitatolewa katika mlango wa Kibla ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya mazazi ya Imamu Hussein (a.s) jioni ya siku ya Alkhamisi tarehe (23/2/2023m) sawa na mwezi (2 Shabani) saa moja jioni.
Aidha kutakuwa na shindano maalum la kuadhimisha mazazi ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha yatafanyika mashindano ya kuzaliwa Imamu Zainul-Aabidina (a.s).