Muhimu.. msafara wa misaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Sirya umeanza

Msafara wa kwanza wa misaada kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu kwenda kwa waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Sirya umeanza.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amesema “Msafara huu ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu, na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, Atabatu Abbasiyya imeanza kutuma msafara wa kwanza wa misaada nchini Sirya kwa ajili ya kusaidia waathirika wa janga la tetemeko la ardhi”.

Akaongeza kuwa “Msafara huo unazaidi ya tani (1555) za chakula na mahitaji mengine muhimu, sambamba na hema watakazo fungiwa waliopoteza nyumba zao kwenye tetemeko, aidha kuna maukibu ya kutoa huduma za chakula”, akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya itatuma msafara mwingine wenye tani (108) za vifaa vya umeme”.

Katibu mkuu akafafanua kuwa “Raia wa Iraq na wahudumu wa Atabatu Abbasiyya wako mstari wa mbele katika kuhudumia binaadamu, hakika nyoyo zao zimejaa huruma na mapenzi ya kweli kwa ndugu zao raia wa Sirya”, akasisitiza kuwa “Atabatu Abbasiyya husaidia watu wenye uhitaji katika maeneo tofauti ndani na nje ya Iraq”.

Mmoja wa wajumbe wa msafara huo Sayyid Muhammad Hamid Majidi amesema “Msafara wa kwanza wenye maroli zaidi ya (70) umeondoka Atabatu Abbasiyya kuelekea nchini Sirya Kwenda kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: