Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya unatoa pongezi kwa wahudumu wa Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (a.s).

Wahudumu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanawapongeza ndugu zao wahudumu wa Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w).

Ugeni huo umeongozwa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Jawadi Hasanawi, wakiwa wamebeba mauwa na kuimba kaswida zinazoashiria furaha kubwa waliyonayo waumini.

Baada ya kuwasili katika malalo ya baba wa watu huru (a.s) wamepokewa na wahudumu wa malalo ya mjukuu wa Mtume (a.s) kwa shangwe na bashasha.

Mshauri wa katibu mkuu katika Atabatu Husseiniyya Sayyid Faadhil Auzi amesema “Jambo hili hufanywa na Atabatu Abbasiyya kila mwaka, huja ugeni maalum hapa Atabatu Husseiniyya kutupa pongezi ya kumbukizi ya watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: