Sayyid Swafi asisitiza utayali wa Atabatu Abbasiyya kusaidia shirika la kusafisha mafuta

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amesisitiza utayali wa Atabatu Abbasiyya kusaidia shirika la kusafisha mafuta.

Ameyasema hayo alipokutana na kiongozi mkuu wa shirika hilo.

Dokta Aaid Jaabir Imrani mkuu wa shirika la kusafisha mafuta amesema kuwa “Tumejadili njia za kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, tukaangalia umuhimu wa hatua inayochukuliwa na selekali ya Iraq ya kufungua kituo cha kusafisha mafuta katika mji wa Karbala chenye uwezo wa kusafisha pipa laki moja na elfu arubaini (140,000) kwa siku, jambo hilo ni mapinduzi makubwa katika sekta ya usafishaji wa mafuta hapa Iraq”, akasema “Kituo hicho kitakuwa na viwango vya kimataifa”.

Akaongeza kuwa “Kituo kipo katika hatua ya majaribio kwa sasa, kitaanza rasmi kufanya kazi mwaka kesho, kinatarajiwa kusafisha mafuta ya dizel kwa kiwango bora zaidi yatakayosaidia kwa kiasi kikubwa mahitaji wa taifa”.

Akabainisha kuwa “Kituo cha usafifaji wa mafuta cha Karbala ni muhimu sana, kitatoa ajira kwa watu wengi sambamba na kupunguza uagizaji wa bidhaa hiyo kwa asilimia (%60 hadi 70) kwa wakati ujao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: