Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya wanafanya tukio la kiibada ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Ratiba hiyo inafungamana na kumbukizi ya kuzaliwa Abulfadhil Abbasi (a.s), wamesimama kwa mistari na kusoma ziara mbele ya kaburi takatifu kisha wakaimba wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Ibaa).
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussawi Ahmadi amesema kuwa “Atabatu Abbasiyya imefanya tukio la kiibada ambalo hufanywa kila mwaka katika siku kama ya leo, ya kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na kufanya shughuli zingine za kuadhimisha kuingia mwezi wa Shabani na Maimamu watukufu waliozaliwa katika mwezi huu”.
Naye mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Rashidi Mussawi amesema “Wahudumu wa Ataba tukufu hufanya tarehe nne ya mwezi wa Shabani katika kila mwaka kuwa siku ya kuhuisha ahadi ya utiifu wao kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kuendelea kutoa huduma hii tukufu waliyotunukiwa na Mwenyezi Mungu ya kuwatumikia Ahlulbait (a.s)”.
Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamesimama mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kusoma qaswida na mashairi yanayo onyesha furaha waliyonayo wafuasi wa Ahlulbait (a.s), kwa kuadhimisha kumbukizi ya watumufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani, aidha kundi kubwa la mazuwaru wa Atabatu Abbasiyya limeshiriki katika ratiba hiyo”