Ugeni kutoka Atabatu Husseiniyya umewasiri Atabatu Abbasiyya katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Wahudumu wa Atabatu Husseiniyya tukufu wamekwenda katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakiwa na mauwa huku wakiimba qaswida na tenzi za kuwasifu Ahlulbait (a.s).
Mshauri wa katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Faadhil Auz amesema “Katika siku hizi tukufu za kuadhimisha watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani, hususan siku aliyozaliwa Abulfadhil Abbasi (a.s), huwa kuna mambo mengi ikiwa ni pamoja na sisi wahudumu wa Atabatu Husseiniyya kuja kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kutoa pongezi”.
Akaongeza kuwa “Ataba mbili tukufu zimekuwa mstari wa mbele kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa kufanya matembezi ya amani, ikiwa ni pamoja na wakati huu wa kumbukizi ya watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani”.
Ugeni wa Atabatu Husseiniyya ulipowasili kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ulipokewa na watumishi wa malalo hiyo kisha wakafanya majlisi ya pamoja, baada ya majlisi wameweka mauwa kwenye dirisha la kaburi takatifu.