Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel inapokea mazuwaru kwa mauwa na halwa

Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya, inapokea mazuwaru kwa kuwapa mauwa na halwa.

Kiongozi wa maendelea ya hatua za Skaut katika jumuiya hiyo Sayyid Alaa Haadi Alhusseini amesema “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, tumeandaa utaratibu wa kugawa mauwa na halwa kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kufuatia maadhimisho ya watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani”.

Akaongeza kuwa “Vikosi vya Skaut tumevigawa katika maeneo manne, upande wa mkoa wa Bagdad, Baabil, Najafu na kikosi cha nne kipo katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: