Kitemgo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kwa kushirikiana na idara ya mradi wa ukanda wa kijani kimefanya maadhimisho ya kuzaliwa kwa mwezi wa familia.
Hafla hiyo imehudhuriwa na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami, makamo rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu na wasimamizi wa mradi wa ukanda wa kijani.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Muslim Shabaki, ikafuatiwa na qaswida na mashairi kutoka kwa kikundi cha waimbaji wa Ahlulbait (a.s).
Miongoni mwa walioshiriki katika uimbaji ni Yaasir Karbalai, Aswili Salami, Alaa Karbalai, Zainul-Aabidina Saidi na Maahir Sultani Rikabi.