Atabatu Abbasiyya yahitimisha hafla za kuadhimisha watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani

Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha hafla za kuadhimisha mazazi ya Imamu Hussein, Imamu Sajjaad na Abulfadhil Abbasi (a.s).

Hafla imehudhuriwa na katibu mkuu wa Ataba tukufu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami, na baadhi ya viongozi na marais wa vitengo pamoja na mazuwaru.

Katika hafla hiyo zimeimbwa qaswida na tenzi za kuwasifu Ahlulbait (a.s), huku mazuwaru wakiweka mashada ya mauwa katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu ilianza kufanya hafla hizo toka siku mbili zilizopita, sambamba na kufanya mashindano yanayohusu watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani.

Atabatu Abbasiyya kupitia vitengo vyake vyote imejiandaa kupokea mamilioni ya nazuwaru watakaokuja kufanya ziara mwezi kumi na tano Shabani, wakati wa kuadhimisha mazazi ya Imamu wa Hujjat msubiriwa (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: