Ujumbe kutoka umoja wa mataifa umepongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Ujumbe kutoka umoja wa mataifa umepongeza mchango mkubwa wa miradi ya Atabatu Abbasiyya katika sekta ya viwanda na kilimo.

Mkuu wa program katika umoja wa mataifa hapa Iraq Sayyid Muhammad Atwaar amesema “Atabatu Abbasiyya inamiliki miradi ya sekta tofauti, inamiradi ya afya, kilimo na viwanda, hakika inahitaji pongezi, kutokana na faida kubwa inayopatika katika miradi hiyo kwa jamii”.

Akaongeza kuwa “Tumejadili namna ya kushirikiana na Atabatu Abbasiyya na kuwapa uzowefu wa kimataifa katika sekta ya umeme na mazingira”.

Mjumbe mmoja kutoka umoja wa mataifa bwana Twariq Muflihu amesema “Tumeangalia mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya elimu, hakika ni fahari kubwa kuwa na taasisi kama hii tukufu”, akasema: “Tunatarajia kuwa na ushirikiano wenye tija na Atabatu Abbasiyya kwa maslahi ya Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: