Makamo rais wa ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Iraq amepongeza huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Makamo rais wa umoja wa mataifa nchini Iraq Mheshimiwa Kalawido Koroduni, amepongeza kazi zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya katika kuhudumia jamii na mazuwaru.

Makamo rais huyo amesikiliza maelezo kutoka kwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini kuhusu kazi zinazofanywa na Ataba tukufu katika kuhudumia jamii na mazuwaru, akaeleza miradi inayotekelezwa na Ataba katika kuhudumia mazuwaru hususan wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Aidha wameangazia umuhimu wa miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya katika sekta ya kilimo, viwanda na elimu kwa kutumia mbinu na vifaa vya kisasa.

Amepongeza miradi ya kimkakati inayolenga kutoa nafasi za kazi kwa vijana wa Iraq, sambamba na kuongeza uchumi wa taifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: