Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wasichana chini ya Atabatu Abbasiyya imehitimisha shughuli za kongamano la Saqaa awamu ya pili.
Kiongozi wa Maahadi Sayyid Manaar Aljaburi amesema: “Kikao cha ufungaji wa kongamano kumefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na qaswida na mashairi kutoka kwa Dokta Ahudi Akili wa Bagdad, halafu ikasomwa risala iliyokuwa na anuani isemayo: (Mbele ya Alkafeel) iliyoandaliwa na idara ya shule za awali za wapenzi wa Alkafeel chini ya Maahadi, kisha mahafidhu (7) wa Qur’ani tukufu wakapewa zawadi na Maahadi”.
Akaongeza kuwa, aidha wamepewa zawadi pia washiriki wa (Nibrasu Aljuud) waliosimamia kikao cha asubuhi, kilichopambwa kwa tenzi na mashairi yanayo onyesha mapenzi na furaha kwa kuadhimisha watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani.
Kikao cha asubuhi kilifunguliwa kwa Qur’ani kisha ikasomwa hutuba ya Imamu Ali (a.s) kuhusu utukufu wa Qur’ani.
Kikosi cha (Nab’ul-Juud) kimesoma Qur’ani kwa pamoja, aidha mwalimu wa Maahadi mwenye umri mkubwa zaidi amepewa zawadi, huku mshairi Rana Khawilidi akisoma qaswida iliyokuwa ikimsifu Abulfadhil Abbasi (a.s).