Chuo kikuu cha Al-Ameed kimefanya hafla kubwa katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na wimbo wa taifa pamoja na wimbo wa Lahnul-Ibaa, kisha washairi wakapanda kwenye mimbari na kuimba mashairi.
Hafla ikapambwa na qaswida kutoka kikundi cha wanafunzi zilizo eleza utukufu wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na ushujaa wao katika kutetea Dini, halafu likafanywa shindano la kielimu.
Hafla ikahitimishwa mbele ya walimu na wanafunzi, waliofaulu kutoa majibu sahihi wakapewa zawadi na mheshimiwa Muayyad Ghazali Rais wa chuo.