Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu imefanya hafla ya (Mimbari za nuru) katika mji mkuu wa Bagdad.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya kupitia kituo cha miradi ya Qur’ani kwa kushirikiana na umoja wa vijana imefanya hafla ya (Mimbari za nuru).

Hafla hiyo imefanywa ndani ya msikiti wa Alhakiim katika mji mkuu wa Bagdad, mbele ya mahafidhu wa Qur’ani tukufu.

Hafla imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa Qur’ani, wasomaji mbalimbali kutoka miradi ya Qur’ani wameshiriki, miongoni mwao ni Mauhubu Hussein Rashidi mmoja wa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, akafuatiwa na msomaji wa Atabatu Alawiyya Sayyid Haani Mussawi.

Hafla ikahitimishwa na msomaji wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Ammaar Alhilly, hafla hiyo ilirushwa moja kwa moja na chenel ya Qur’ani katika luninga ya Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: