Sayyid Swafi ametembelea Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu na amepongeza miradhi inayofanywa.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ametembelea Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa-Ilmi ya Qur’ani katika Ataba tukufu.

Mheshimiwa amepongeza ratiba na miradi ya Qur’ani inayofanywa na Maahadi, akasisitiza umakini katika kazi na kubuni miradi yenye athari katika jamii.

Akaongeza kuwa “Hakika tunapongeza kazi nzuri inayofanywa na Maahadi ya kufundisha Qur’ani katika jamii sambamba na kulea wasomi wa Qur’ani na wanafunzi wa hauza”.

Mkuu wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali amesema “Kiongozi mkuu wa kisheria Ameangalia huduma zinazotolewa na Maahadi ambazo zinalenga kutengeneza kizazi cha wasomi na mahafidhu wa Qur’ani tukufu, pamoja na mradi wa Tablighi unaohusisha mikoa yote, bila kusahau ratiba ya Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi na uendeshaji wa mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur’ani kwa watu wa tabaka zote na umri tofauti”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: