Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza kuanza kwa shindano la kitamaduni awamu ya nne linalohusu watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani hususan Imamu Mahadi (a.f).
Shindano limepewa jina la (watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani), shindano hilo linafanywa sambamba na maadhimisho ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) waliozaliwa katika mwezi wa Shabani.
Majina ya washindi kumi wa mwanzo yatatangazwa saa nne asubuhi siku ya Ijumaa ya tarehe (3/3/2023m) kwenye majukwaa ya mawasiliano ya kijamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Sharti la kupokea zawadi ya ushindi, mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla itakayo fanywa katika eneo la mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Ijumaa (3/3/2023m) saa moja jioni.