Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amesema kuwa, program ya mabinti wa Alkafeel ni msaada mkubwa kwa mwanamke wa Kiislamu, inamsaidia kutekeleza wajibu wake kwa taifa.
Mheshimiwa katibu mkuu amesema “Hafla ya wanafunzi wa kike wanaohitimu vyuo vikuu vya Iraq ni sehemu ya msaada kwao pia, inasaidia kuwafundisha mambo muhimu yanayohusu ujenzi wa familia na kutekeleza wajibu wa kimaadili na kibinaadamu na mkakati wa taifa”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imepokea wanafunzi kutoka mikoa tofauti, waliokuja kufanya hafla ya kuhitimu masomo yao mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na safari yao ya kazi kuanzia mahala hapa patakatifu”.
Akaendelea kusema kuwa “Kwa mwaka wa tano mfululizo Atabatu Abbasiyya tukufu imekuwa ikifanya hafla hii kwa mabinti zetu, chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi”, akabainisha kuwa “Jina la (mabinti wa Alkafeel) limechaguliwa kutokana na utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.