Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amemzawadia mshindi wa pili wa shindano la kimataifa la usomaji wa Qur’ani tukufu, bwana Osama Karbalai.
Sayyid Ahmadi Swafi akasisitiza kuwa Atabatu Abbasiyya inasaidia kila aina ya vipaji vya Qur’ani, aidha amemuhimiza kuendelea kushiriki kwenye mashindano ya Qur’ani ya kimataifa, kwa lengo la kuinua jina la Iraq na Ataba tukufu.
Mheshimiwa amesisitiza kuwa semina za Qur’ani zinatakiwa zisiishie kwenye kusoma na tafsiri tu, bali zinatakiwa zipanue wigo zaidi katika masomo ya Fiqhi, Aqida, Akhlaq yaani ziwe pana zaidi.
Karbalai anasema “Amepewa zawadi baada ya kupata nafasi ya pili kwenye mashindano ya Qur’ani ya kimataifa yaliyofanyika nchini Qatar jumla ya nchi (70) zilishiriki”.
Hafla ya kukabidhi zawadi imehudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu Sayyid Jawadi Hasanawi na rais wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu Dokta Mushtaqu Ali.