Atabatu Abbasiyya imetangaza majina ya waliofaulu kwenye shindano la kitaifa la ujuzi wa uhadhiri awamu ya saba.

Kamati ya majaji wa shindano la ujuzi wa uhadhiri awamu ya saba, linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza majina ya washindi.

Shindano hilo limesimamiwa na idara ya mahusiano ya vyuo na shule, kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel.

Aliyeshika nafasi ya kwanza ni Muhammad Farasi Twaha kutoka idara ya malezi ya mkoa wa Misaan, nafasi ya pili ikashikwa na Omari Mushtaaq Haamid kutoka idara ya malezi ya mkoa wa Swalahu Dini.

Nafasi ya tatu ikishikwa na Abdullahi Muhammad kutoka idara ya malezi ya mkoa wa Bagdad, na nafasi ya nne akashikwa na Twaha Athumani Dhunuun kutoka mkoa wa Nainawa, nafasi ya tano akashinda Ayubu Abduswamad kutoka Bagdad.

Shindano hilo limefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) na limedumu kwa muda wa siku mbili, jumla ya idara ishiriki kutoka mikoa tofauti ya Iraq zimeshiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: