Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake imetangaza kuhitimu masomo kwa wanafunzi 55 wa masomo ya Qur’ani na hukumu za usomaji.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imetangaza kuhitimu kwa wanafunzi (55) walioshiriki semina za usomaji wa Qur’ani tukufu zilizofanywa na Maahadi.

Kiongozi wa Maahadi Ustadhat Maraar Aljaburi amesema “Kamati maalum ya walimu wa Maahadi imewapa mtihani wanafunzi (55) waliohitimu semina za Ahkaamu-Tajwidi, wanafunzi wote wamefanya vizuri kwenye mitihani yao”.

Akabainisha kuwa, wahitimu wa safari hii ni wanafunzi kutoka shule na vyuo vikuu, Maahadi inafungua milango yake daima kwa ajili ya kupokea wanafunzi wapya wanaotaka kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: