Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na mradi wa (mauwa ya Faatwimiyya) awamu ya tano.
Bibi Maha Ahadi Abdu Zuhrah mmoja wa wahudumu wa idara amesema “Mradi unalenga kuwaandaa wanafunzi wa shule katika kutelekeza wajibu wa Dini na majukumu ya kisheria, awamu ya tano imejikita kwenye shule zilizopo pembezoni mwa mji wa Karbala”.
Akaongeza kuwa “Mradi unalenga idara ya shule ya Maryam-Adhraa, kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi kusoma surat Faat-ha kwa njia sahihi, na namna ya kutawadha na kuswali pamoja na kushikamana na hijabu ya kisheria ambalo ni vazi la lazima kwa mwanamke wa kiislamu”.
Mradi huu unafanywa kwa kushirikiana na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala, wazazi na viongozi mbalimbali hapa mkoani wamepongeza sana mradi huu.