Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimefanya maonyesho ya vitabu katika mkoa wa Basra.
Maonyesho hayo yamesimamiwa na kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo, kwa kushirikiana na idara ya malezi ya Basra.
Maonyesho yamefanywa ndani ya ukumbi wa Ridhwani katika wilaya ya Shatul-Arabu, kundi kubwa la wanafunzi wa sekondari limeshiriki, maonyesho yamesaidia kutambulisha historia ya mji wa Basra na turathi ilizonazo.
Maonyesho yalikuwa na vitabu vingi vilivyo chapishwa na kituo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, bango mbalimbali, picha zinazoonyesha mazingira tofauti ya mji wa Basra pamoja na nakala kale adimu zilizo andikwa na wanachuoni wa Basra katika miongo tofauti.