Vituo vya mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu vimepata muitikio mkubwa wa mazuwaru.

Vituo vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu kwa mazuwaru, vimepata muitikio mkubwa kutoka kwa watu wanaokwenda Karbala kufanya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani.

Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa-Ilmi katika Atabatu Abbasiyya imefungua vituo vya kufundisha Qur’ani kwa mazuwaru.

Vituo hivyo vimefunguliwa kwenye barabara ya (Karbala – Baabil), walimu wanafundhisha usoamaji sahihi wa surat Faat-ha, sura fupifupi na nyeradi za swala kwa watu wasiojua kusoma, mazuwaru wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa huduma hii tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: