Jopo la madaktari limefanikiwa kuondoa uvime kwenye ubongo wa mgonjwa katika hospitali ya rufaa Alkafeel

Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel, limefanikiwa kuondoa uvimbe kwenye ubongo wa mgonjwa uliokuwa unatishia uhai wake.

Rais wa jopo hilo, Dokta Ahmadi Adnani amesema “Mgonjwa alikuwa na tatizo la uvimbe kwenye ubongo uliopelekea kuwa na maumivu makali ya kichwa, tatizo hilo lilijulikana baada ya kufanyiwa vipimo”.

Akaongeza kuwa “Jopo la madaktari wetu limefanikiwa kuondoa uvimbe kwenye ubongo kwa kutumia mtambo wa kisasa”.

Upasuaji wa aina hii hauwezi kufanywa ispokua kwenye vituo maalum, kwani unahitaji mitambo maalum, akasisitiza kuwa “Mgonjwa ataanza kutembea na kurudi katika hali ya kawaida siku ya tatu baada ya kufanyiwa upasuaji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: