Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Sistani leo siku ya Alkhamisi, amepokea ugeni kutoka Vatkan.
Tamko kutoka ofisi ya Sayyid Sistani linasema kuwa “Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Sistani amepokea ugeni kutoka Vatkan ukiongozwa na rais wa baraza la Papa Kadinali Mikael Anjelo Ayuzo Ghikso na wamefanya mazungumzo kuhusu maswala ya Dini”.
Kadinali Ghikso amewasilisha “Ujumbe maalum wa shukrani kutoka kwa Papa Fransis katika kumbukizi ya mwaka mmoja tangu alipokaribishwa katika mji wa Najafu”.
Tambuwa kuwa ujumbe wa Papa unaundwa na “Rais wa baraza la Papa anayehusika na kitengo cha mahusiano ya kidini, katibu wa kamati ya Markosi Solo na katibu wa ubalozi wa Vatkan nchini Iraq mheshimiwa Suna”