Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya semina ya Qur’ani katika mkoa wa Baabil.
Semina hiyo inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani ya Baabil chini ya Majmaa.
Mkufunzi wa semina hiyo ni Dokta Raaid Qassimi, amefundisha hukumu za usomaji wa Qur’ani, umuhimu wa lugha ya kiarabu katika utamkaji kwa ufasaha wa maneno matakatifu ya Mwenyezi Mungu na kujiebusha na lahaja za kiarabu wakati wa usomaji wa Qur’ani.
Semina hii ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Qur’ani unaolenga Maahadi na vyuo vya Iraq, Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Baabil imeandaa zawadi kwa washiriki na vyeti vya ushiriki pamoja na safari za kidini kwa wanasemina, aidha washiriki wa semina hii watapewa nafasi ya kushiriki katika semina zijazo.