Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi, amesema kuwa fatwa tukufu ya kujilinda ilibadilisha mambo kwa ujumla.
Ameyasema hayo kwenye ujumbe aliotoa wakati wa ufunguzi wa kongamano la Ainul-Hayaa linalosimamiwa na taasisi ya Qabsu ya utamaduni na maendeleo.
Sayyid Swafi amesema “Fatwa tukufu ilipata muitikio mkubwa sana hadi kwa vijana wadogo ambao hawajabalekhe”, akafafanua kuwa “Fatwa ilileta mabadiliko ya kweli yaliyo badilisha mambo yote kwa ujumla”.
Mheshimiwa akafafanua kuwa “Ardhi ya Iraq inamatukufu mengi na fatwa hiyo ni urithi mzuri katika historia ya kujitolea”.
Akaendelea kusema “Marjaa Dini mkuu alitumia njia nzuri sana ya kupambana na makundi ya magaidi katika wakati ambao njia zote zilikua zimefeli, hakika fatwa hiyo tukufu ilizima ndoto za wale waliotarajia ushindi unaweza kupatikana baada ya miaka thelathini”.