Kongamano hilo hufanywa kwa kushirikiana baina ya kitengo cha habari na utamaduni na taasisi ya Waafi inayojishughulisha na tafiti katika Atabatu Abbasiyya.
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Sayyid Ahmadi Swadiq amesema “Shindano litafwanywa wakati wa kongamano la awamu ya saba chini ya kauli mbiu isemayo (Marjaa Dini ni ngao ya umma wa kiislamu) tarehe mbili mwezi wa sita”.
Akaongeza kuwa “Shindano hilo ni kwa ajili ya kukusanya vielelezo vya mambo yaliyotokea wakati wa vita na ushujaa uliofanywa na wananchi watukufu katika kukomboa ardhi zao kutoka kwa magaidi, na uwe ni ukumbusho kwa vizazi vijavyo”.
Ili uweze kushiriki kwenye shindano hili unatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo:
- Kipande cha filamu kiendane na kauli mbiu ya kongamano, na kiwe kinauwiyano na vipengele vyake.
- Filamu ionyeshe ushujaa wa jeshi la Iraq na Hashdu Shaabi kwa ujumla (bila kulenga muelekeo maalum) katika kulinda taifa, misingi ya ubinaadamu na maeneo matakatifu.
- Filamu isiwe imeshawahi kuonyeshwa na chombo chochote cha habari au kushiriki kwenye mashindano mengine.
- Filamu iwasilishwe kwenye taasisi ya Waafi katika Atabatu Abbasiyya ikiwa na wasifu (cv) ya muandaaji, au utumwe kwenye toghuti ya kimataifa Alkafeel (www.alkafeel.net).
- Tunaanza kupokea filamu tarehe (10/03/2023m) hadi (15/05/2023m).
- Muda wa filamu usiwe chini ya dakika moja (1) wala sio usizidi dakika kumi (10).
- Filamu itengenezwe kwa mfumo wa (HD) au (AVI).
- Kwa maelezo zaidi kuhusu shindano tupigie simu namba (07706000506).
Washindi watatu wa mwanzo watapata zawadi kama ifuatavyo:
- 1- Mshindi wa kwanza 3,000,000 milioni tatu dinari za Iraq na ngao.
- 2- Mshindi wa pili 2,000,000 milioni mbili dinari za Iraq na ngao.
- 3- Mshindi wa tatu 1,000,000 milioni moja dinari za Iraq na ngao.