Kitengo cha maarifa kinazipa vitabu taasisi za utamaduni katika mji wa Dhiqaar

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimezipa vitabu taasisi za Maktaba katika mji wa Dhiqaar.

Jambo hilo limefanywa chini ya mpango wa ushirikiano baina ya kituo na taasisi za kitamaduni, kielimu na maktaba za hapa mkoani.

Ugeni umetembelea kituo cha turathi za kusini chini ya kitengo kikuu cha maktaba, na kukutana na mkuu wake Sayyid Twalibu Hasanawi, aidha wakatembelea maktaba ya chuo kikuu cha Dhiqaar na kukutana na mkuu wa maktaba hiyo Dokta Maajid Jamiil Zuhairi, ameshukuru kituo kwa kazi nzuri kinayofanya katika sekta ya turathi na tafiti.

Maktaba ya Imamu Baaqir (a.s) ilikuwa na umaalum wake katika jengo la Shekhe Abbasi Alkabiir, iliandaliwa vitabu rasmi, ujumbe ulikutana na kiongozi wa maktaba Shekhe Raad Naashii, na wakakubaliana kuendeleza mawasiliano kwa faida ya pande mbili.

Kituo cha turathi za kusini kinafanya juhudi kubwa ya kugawa machapisho yake (vitabu) na nyaraka za turathi za kusini kwenye maktaba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: