Chuo kikuu cha Alkafeel chuni ya Atabatu Abbasiyya kinafanya mihadhara kuhusu njia za kisasa katika ufundishaji wa udaktari.
Ratiba hiyo imesimamiwa na kitivo cha udaktari kwa kushirikiana na idara ya elimu endelevu.
Miongoni mwa wahadhiri ni mbobezi wa elimu ya tiba Dokta Hilali Swafaar na mbobezi wa famasia Dokta Yasimini Ali, mihadhara imetolewa mbele ya rais wa chuo, wakuu wa vitengo na walimu wa chuo.
Mihadhara ilijikita katika kueleza mbinu za kisasa za ufundishaji na malengo ya elimu.
Swafaar amesifu ushirikiano mkubwa uliokuwepo baina ya watendaji chini ya chuo kikuu cha Alkafeel, akasema jambo hilo ni muhimu katika safari ya elimu.