Makumbusho ya Alkafeel inashiriki kwenye maonyesho maalum yanayofanyika pembezoni ya kongamano la (Ainul-Hayaa).
Muwakilishi wa makumbusho katika kongamano hilo Sayyid Imaad Tamimi amesema “Makumbusho ya Alkafeel inashiriki kwenye maonyesho ya kongamano la (Ainul-Hayaa) linalosimamiwa na taasisi ya Alqabsu kwenye uwanja wa makumbusho jijini Bagdad, kongamano hilo linalenga kuinua kiwango cha utamaduni na utunzaji wa makumbusho katika jamii ya wairaq hususan tabaka la vijana”.
Akaongeza kuwa “Kwenye maonyesho hayo zimeonyeshwa mali-kale zinazowakilisha zile zilizopo kwenye makumbusho iliyopo ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Tamimi akabainisha kuwa “Mali-kale zilizo onyeshwa ni baadhi ya vipande vya dirisha jipya la Abulfadhil (a.s) na baadhi ya mali-kale ambazo historia yake inarejea miongo tofauti, baadhi ya ngao, miswala ya kihistoria pamoja na kuelezea namna ya kukarabati mali-kale zilizoharibika”.