Hospitali ya Alkafeel imeonyesha mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya matibabu.

Maonyesho ya kongamano la Ainul-Hayaa la kimataifa linalofanywa katika ardhi ya Bagdad, hospitali ya rufaa Alkafeel imeonyesha mafanikio yake katika sekta ya matibabu.

Kiongozi wa uhusiano katika hospitali hiyo Sayyid Hassan Aaridhwi amesema, “hospitali ya Alkafeel imeshiriki kwenye banda la Atabatu Abbasiyya kwenye maonyesho yanayo endelea jijini Bagdad na imeonyesha mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya afya”.

Akaongeza kuwa “Hospitali imeonyesha mafanikio yake kwenye sekta ya matibabu, na upasuaji uliokuwa mgumu kufanywa ndani ya Iraq, ambao leo unafanywa katika hospitali ya Alkafeel chini ya madaktari wa kiiraq”.

Maonyesho ya kongamano la Ainul-Hayaa awamu ya kwanza yamehitimishwa jana, jumla ya matawi (17) ya Atabatu Abbasiyya tukufu yameshiriki kwenye maonyesho hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: