Chuo kikuu Alkafeel kinafanya nadwa ya kielimu kuhusu hatari za dawa za kulevya katika chuo cha Kufa

Wataalamu kutoka chuo kikuu cha Alkafeel wanafanya nadwa katika chuo kikuu cha Kufa inayohusu hatari za dawa za kulevya yenye anuani isemayo (Athari za kutumia dawa za kulevya na hatua za kujiebusha nazo).

Katika nadwa hiyo mada za kitafiti zimewasilishwa na Dokta Ahmadi Hashim Rifai na Dokta Husaam Ali Ubaidi, aidha ameshiriki pia dokta Hiyaam Hassan kutoka chuo kikuu cha Kufa, kwa kutoa (takwimu za matumizi ya dawa za kulevya).

Watafiti wakaendelea kueleza madhara ya dawa za kulevya katika jamii, na sababu ambazo hupelekea watu kuingia katika janga hilo, miongoni mwa sababu hizo ni matatizo ya kifamilia, mpasuko katika familia na vijana kutotumia muda wao katika kusoma na michezo.

Watafiti wakafafanua kwa undani madhara ya kiafya anayopata mtu anayetumia dawa za kulevya.

Uongozi wa chuo kikuu cha Kufa ukapongeza na kushukuru juhudi zinazofanywa na wataalamu kutoka chuo kikuu cha Alkafeel na mafanikio makubwa yanayopatikana kutokana na juhudi zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: