Balozi wa Krashia nchini Iraq amepongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya ya afya na elimu

Balozi wa Krashia nchini Iraq Mheshimiwa Ifani Yorish, amepongeza miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, katika sekta ya afya, elimu na zinginezo.

Yorish alipotembelea malalo takatifu siku ya Jumanne na kuangalia miradi ya Atabatu Abbasiyya kisha akasema “Ninafuraha kubwa kuona maendeleo mazuri ya mji huu, hususan mtazamo bora uliopo kwa uongozi mkuu wa Ataba tukufu na kufanya miradi ambayo matunda yake hayaishii kwa watu wa Karbala pekeyake bali mikoa yote ya Iraq”.

Akaongeza kuwa “Miradi hiyo ni muhimu sana hasa inayohusu sekta ya afya, elimu na mingineyo ambayo inanufaisha mji wa Karbala na Iraq kwa ujumla”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: