Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa ziara ya malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) na Maraajii watukufu kwa wahudumu wake.
Kiongozi wa ujumbe huo Shekhe Maajid Sultwani amesema “Ziara hiyo inaimarisha mahusiano kati ya wahudumu hao na wale wa malalo zingine, aidha ziara hii ni sehemu ya motisha kwa wahudumu kutokana na kazi kubwa wanayofanya”.
Akaongeza kuwa “Ziara haikuishia kuzuru malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) peke yake, bali tumetembelea ofisi za Maraajii Dini watukufu kwa ajili ya kujenga mahusiano na kupata muongozo wao na usia wao mtukufu, tumewaahidi kufuata maelekezo yao na kufanyia kazi miongozo yao”.
Akafafanua kuwa “Tulikuwa na kikao kirefu na Marjaa-Dini Ayatullahi Shekhe Bashiru Najafi, baada ya mapokezi mazuri aliyotupatia alitoa nasaha nzuri na kutaja neema na baraka wanayopata wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.