Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inafanya semina katika fani ya adhana na misingi yake kwa waadhini wa misikiti ya Baabil.
Semina hiyo inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majmaa.
Mkuu wa Maahadi Sayyid Muntadhar Mashaaikhi amesema “Maahadi inafanya semina kuhusu adhana na misingi yake kwa waadhini wa misikiti ya Baabil, masomo yamejikita katika sauti, naghma, mitindo ya kuadhini na mambo mengine yanayohusu fani hiyo”.
Akaongeza kuwa “Katika semina hiyo ambayo mkufunzi wake ni Muhsin Rimahi inazaidi ya washiriki thelathini, itadumu kwa muda wa siku kumi mfululizo”.
Wanafundishwa namna ya kuadhini kwa ufasaha na misingi ya naghma pamoja na mambo mengine ya msingi katika adhana, kwa mujibu wa maelezo ya Mashaaikhi.