Atabatu Abbasiyya imesisitiza kuwa itahakikisha miradi ya kilimo na viwanda inasaidia kupunguza tatizo la ajira.

Mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami, amesema kuwa miradi ya kilimo na viwanda itasaidia kupunguza tatizo la ajira katika jamii.

Ameyasema hayo katika ujumbe aliotoa wakati wa kuhitimisha kongamano la kielimu la 16 katika chuo kikuu cha Karbala, kwenye mkutano uliofanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Akasema kuwa “Hakika Ataba tukufu za Iraq hususan Ataba mbili za Husseiniyya na Abbasiyya zimekuwa na miradi mingi ya kijamii, kama viwanda, kilimo, afya, elimu, miradi ambayo inaweza kupunguza tatizo la ajira katika jamii kwa kiwango kikubwa”.

Akaongeza kuwa “Huduma zinazotolewa na taasisi za Ataba zipo za aina mbili, kwanza huduma za kiroho kwa mazuwaru nazo hutolewa ndani ya haram za Ataba tukufu, sehemu ya pili huduma za kijamii kama vile miradi ya viwanda, kilimo, afya na elimu”.

Akabainisha kuwa “Vituo vya afya na hospitali zilizojengwa na Ataba tukufu zimesaidia sana kuepusha safari za kwenda kutibiwa nje ya Iraq, ukizingatia kuwa wananchi wengi hawana uwezo wa kwenda kutibiwa nje ya nchi, Ataba zimejitahidi kuajiri madaktari bingwa na kuwa na vifaa-tiba vya kisasa vinavyo wezesha kufanya huduma ya upasuaji wa kila aina hapa nchini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: