Ugeni wa sekula kutoka Dhiqaar unaangalia miradi ya Atabatu Abbasiyya ya utoaji wa huduma na afya.

Ugeni wa kisekula unaohusisha walimu wa chuo na wanafunzi kutoka wilaya ya Shurtwa, unaangalia miradi ya Atabatu Abbasiyya kupitia ratiba iliyoandaliwa na kitengo cha mahusiano.

Mhadhiri wa chuo Sayyid Jasaam Saidi amesema “Kupitia ratiba ya Atabatu Abbasiyya ya kupokea wageni kutoka vyuo vikuu na taasisi za kielimu, tumepokea wageni kutoka kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Dhiqaar”.

Akaongeza kuwa “Lengo la ratiba hiyo ni kuangalia miradi ya Ataba, kikiwemo chuo kikuu cha Al-Ameed na hospitali ya Alkafeel sambamba na kusikiliza mihadhara ya kielimu”.

Akaendelea kusema “Wageni wameangalia mafanikio ya Atabatu Abbasiyya katika utoaji wa huduma, hakika Ataba imekuwa mfano mzuri wa kuigwa kitaifa na kieneo”.

Wageni wamefurahishwa na miradi ya Ataba tukufu, hususan miradi ya afya, kutokana na vifaa-tiba vya kisasa vilivyopo na huduma bora wanayotoa kwa jamii ya raia wa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: