Kwa ushiriki wa mahafidhi (100) Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake inafanya shindano la Qur’ani la Fedha.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya shindano la Qur’ani la Fedha awamu ya tano lenye washiriki (100) waliohifadhi Qur’ani tukufu.

Kiongozi wa Maahadi Ustadhat Manaar Aljaburi amesema “Baada ya kufanya mashindano kwenye matawi yake, leo inafanya shindano katika mkoa wa Najafu likiwa na washiriki (100) lililopewa jina la Fedha kama sehemu ya kumuenzi mtumishi wa bibi Zaharaa (a.s) bibi Fedha”.

Akaongeza kuwa “Wanafunzi wanaoshiriki kwenye shindano la Fedha wakochini ya umri wa miaka (18)”.

Akabainisha kuwa “Shindano hili linafanywa ndani ya ukumbi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu, kila siku kunavikao viwili cha asubuhi na jioni”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: