Ugeni kutoka chuo cha Malkiwa wa Wingereza unaangalia maandalizi ya mitihani ya udaktari kwa wanafunzi wao.

Ugeni kutoka chuo cha Malkia wa Wingereza umetembelea maeneo ya chuo kikuu cha Al-Ameed na hospitali ya rufaa Alkafeel, kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya mitihani ya udaktari kwa wanafunzi wake.

Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Dokta Jaasim Saidi Ibrahimi amesema “Mitihani ya chuo cha Malkia wa Wingereza itafanywa Iraq, zamani ilikuwa inafanywa Injiltara, hili ni tukio la kimataifa, ukizingatia kuwa mitihani hiyo itafanywa kwa usimamizi wa hospitali ya rufaa Alkafeel na chuo kikuu cha Al-Ameed, chini ya Atabatu Abbasiyya katika mkoa wa Karbala”.

Akafafanua kuwa “Hospitali na chuo vikotayali kwa ajili ya mitihani haiyo, jambo hili linaweka sifa nzuri ya kielimu na ubora wa huduma tunazotoa”.

Kwa mujibu wa Ibrahimi “Ugeni umetembelea chuo cha Al-Ameed na hospitali ya rufaa Alkafeel jana siku ya Jumamosi”.

Akasema “Haya ndio matarajio ya Atabatu Abbasiyya tukufu, lengo letu sio kutoa huduma bora peke yake, bali kuwa kituo bora zaidi katika utoaji wa huduma na elimu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: