Kuanza kuwasiri wanafunzi wanaoshiriki kwenye hafla ya mauwa ya Faatimiyya.

Wanafunzi wa shule tofauti katika mkoa wa Karbala wameanza kuwasiri katika jengo la Shekhe Kuleini kwa ajili ya kushiriki kwenye hafla ya “Mauwa ya Faatwimiyya” awamu ya tano.

Wanafunzi wanawasiri kwa makundi kuja kushiriki kwenye hafla hiyo inayosimamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na idara ya malezi ya Karbala.

Hafla itakuwa na vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya na kipengele cha mashairi, hafla hiyo inafanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu ndio utambulisho na ujumbe wangu), aidha kutakuwa na igizo lisemalo (punda na shetani) na video inayo onyesha mradi wa mauwa ya Faatwimiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: